KIOO CHA MZALENDO
KIOO CHA MZALENDO
Najua it has been a long time
Ever since niongee
kuhusu politics
BUT, naweza chelewa kusema
Lakini kalamu haitachelewesha mistari
Bora nisipatikane behind bars
I want to reflect kile
Kioo changu kimemulika tangu tupate UHURU
Kweli, si tulipata UHURU tukakuwa na UHURU kisha
tukakosa UHURU
Wajinga sisi.
Najua hadi story ya Hague mulisahau
Tunangoja kuona washtakiwa wakiendelea na kesi
But, this can’t be a reality
Kwani sisi ndowashenzi
Watu dynasty si wanajua kucheza kivyao
Na kila kitu kuwekwa under water
Time ya election
Kura tunapiga kuchagua viongozi
Ambao walishajipatia uongozi
na, wanangojea
kuapishwa rasmi
si ni sisi vipofu.
Uchochezi wa siasa ukitoka si ni raia anaumia
vifo vya watu innocent kama Pendo ndo tunasikia
Evidences zafichwa
maiti kupatikana bila fingers
Vituo vya habari zafungwa
Taarifa isisambae
Huku tukisema tulipata UHURU
Wajinga sisi.
Janga mbalimbali zatokea
Mafuriko, locust and now CORONA
Sijui more kuihusu coz,
Habari zake ni kama zile za,
Hide and seek games
For us ni ihari tujilinde
TUSANITIZE, TUVAE MASK, NA TUKEEP SOCIAL DISTANCE.
Hadithi za BBI zikachipuka
MCAs wakaahidiwa 2 million kuisupport
Swali, kama ni halali mbona itolewe hongo?
Nurses wamegoma wanataka mishahara
Bilioni moja imepotea sijui wapi
Uchumi unapanda, deni tunazo
Lakini hongo ya siasa ipo.
Pesa zapotea idadi kubwa but,
Hizi story zapotea very first
Hatuskii wakitangaza BANK HEIST
Kwani, hizi pesa zapotea wapi
Deni China tunayo gaha
Tax zapandishwa kulipa deni
Habari tunazo
Lakini hatusikii zimelipwa kiasi gani
Ama sisi ndo viziwi!
Gharama ya maisha imefika ng’ambo,
tungali nchini mwetu
Kufill gas bei imepanda
kama
accelerator ya kuenda 12th floor
Mafuta bei imepanda
twalalamika lakini
vilio vyetu havisikiki,
Ama ni vile vya bubu na vipofu hawaoni
Msisahau ahadi za 10 years ago
Laptops, masomo ya bure,
Lakini tunachopata ni mkono mtupu
Au, ahadi hizo zilipeperushwa na upepo
Sasa tena wheelbarrows na mikokoteni
Yani siasa ikiwadia raia ni kitumizi tu!
Wajinga sisi.
HUDUMA number tulichukua
Umuhimu wao ukawa upi,
Pendekezo za siasa twazitii lakini hatuelewi
Ndo maana nasema, TULIKOSA UHURU.
Reviewed by Kenn the Poet
on
June 22, 2021
Rating:


No comments: