JUAKALI
Juakali Mimi Juakali
Heshima nami utanipa
Chepeo lazima utaivaa
Mwavuli utanunua
Kivulini utaketi
Sababu Mimi ni Juakali.
Juakali Mimi Juakali
Mbona mwanidhulumu mie?
Asubuhi na mapema safarini nipo
Mchana yote kwenye Juakali
Jasho natokwa riziki nipate
Mchafu mie, takataka mwanifananisha.
Juakali Mimi Juakali
Nisipongaa mngali baridi
Maganjwa mtayapata
Lishe na siha njema mtaikosa
Heshima yangu mtanipa.
Juakali Mimi Juakali
Mali zangu sharti mwahitaji
Mbona Hela mwanipuja?
Wazimu mwanilinganisha
Tafadhali, mie pia adhamu.
Mimi Juakali heshima Nampa Juakali
Asubuhi kabla ya Juakali
Naraukia Juakali lishe kwa aushi nipate
Bidhaa zangu naziweka kwa Juakali
Heshima zangu mupokee wenzangu Juakali
# Milcah the Poetess
@ Kenyan Mind Speak.
No comments: