HONGERA DADA
Bintiye mwenye heshima ,ee Mungu akubariki
Kitisiti kasimama,wanadamu wahakiki
Walosema utazama,wote sasa ni shabiki
Tabasamu uwapee ,usiwe nao na chuki.
Shuleni ulieenda,baba katoka ghafula
Wakanena hutaenda ,bahati kaja ghfula
Mama kasema taenda,wadaku waone bala
Tabasamu uwapee,usiwe nao na chuki
Inne miaka kapita ,dato inne kamaliza
Kijiji basi katoka, akili enda tuiza
Gange kaenda tafuta ,zahela hujamaliza
Tabasamu uwapee,usiwe nao na chuki
Maadui kakujia ,walidhani tashindwa
Akilini kaamua ,kamwe hutashindua
Riziki jitafutia ,maadui watadua
Tabasamu uwapee,usiwe nao na chuki
Maurine lako jina,sijui lake maana
Kweli basi tang'ang'ana, kujua lake maana
Heshima wako maana,baraka kwako kwa pana
Tabasamu uwapee , usiwe nao na chuki
Wako mgeni kawasili, jina Darliah ukampa
Kwa shairi taasili,hongera nami takupa
Wambea iwaasili,aibu kweli mewapa
Tabasamu uwapee,usiwe nao na chuki
Nina mengi kuwaambia,kwa kifupi takatia
Beti saba malizia,bali sitanyamazia
Hongera dada pokea, kweli we wajishindia
Tabasamu uwapee,usiwee nao na chuki.
Reviewed by Milcah the Poetess
on
December 20, 2020
Rating:

No comments: